[.:ENGLISH:.|.:ITALIAN:.|.:FRENCH:.|.:SWAHILLI:.|.:HINDI:.    
 
 


 

News letter subscription
   
Name
Email
 

 

 

 

 

 

 

 

 

SIRI YA LAANA YAKE HAMU

PDF

Mwanzo 9:20-27
20Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25Akasema, Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26Akasema, NA atukuzwe Bwana, Mungu wa Shemu; NA Kanaani awe mtumwa wake.
27Mungu akamnafisishe Yafethi, NA akae katika hema za Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.

Napata kutambua siri hii ya laana yake Hamu, kuwa moja ya funuo kuu zaidi ambazo Bwana anafunua kwetu sisi kupitia bibilia. Ukaweza kuipata hii siri, na kuielewa, utapata kujivika mabawa ya Roho na ukaweze kupaa tena kurudi utukufuni. Hii siri sio maziwa ya kiroho kwao watoto katika roho, mbali ni chakula kigumu kwao wana ambao wanazidi kusonga hadi tamati ya ukamilifu wa utukufu wake Mungu. Kama utapata mambo fulani katika  maandishi haya ambayo hayako bayana kwako, basi ukaweze kumwomba Baba wa Nuru akaweze kukupanua katika kuelewa kwako na ufahamu wako, Naye atakupa. Kwa kuwa ni mapenzi Yake kukutia Nuru ya Uzima wewe na kila mtu duniani.

“Laana ya Hamu” ni jambo linalojulikana na wengi walio na fikra za kidini, haswa wale walio wa uzao wa Kiebrenia. Bila kujulikana na wengi, dini ya Waebrania ilioanzishwa naye Musa imeenea na sasa ni msingi ya dini zingine nyingi (dini ya Kikristo ikiwemo) na misingi mingine mingi ya kiserikali, sheria, na husiano tofauti ulimwenguni kote. Hapo kale, misingi hii, ilipojaribu kutafuta wale walio wa uzao wa Hamu, ilielekea katika vilindi vya walio Afrika na hata kudhania kuwa Waarabu ndio wana wa Hamu. Kwa imani hii, utumwa na ubaguzi wa rangi kuwaelekea walio ngozi nyeusi ulienea  karne ya kumi na nane hadi ya ishirini. Lakini imekuwa ikipunguzwa tulipopita karne ya ishirini. Na kwa hakika, kule nje, kuna uwezekano kuwa kuna watu na mataifa yalio uzao wake Hamu, ambao wanawezakuwa bado wako chini ya laana ambayo Nuhu alimtwika mwanawe. Lakini tilia hili maanani; huu sio ujumbe uliokuwa uletwe kwetu kupitia laana ya Hamu; Ufunuo ulioko pale ni mpana na mkuu zaidi kuliko vile.

Kwanza, laana ya Hamu ingiwezafanya kazi kwa sababu mwanadamu tayari alikuwa chini ya laana pale mwanzo. Picha kuu ilioko ni kuwa wanadamu wote kama tujuavyo wamepungukiwa na utukufu wa Mungu na wanagaagaa chini ya laana ya sheria. Mapenzi yake Baba ni kuwakusanya wanadamu WOTE kutoka kwa adhari za laana; na Mungu akitufungua vile, hizi laana dhaifu zinazopatikana katika ile laana ile ya kwanza, kama hii ya Nuhu kwa mwanawe hazitakuwa na adhari yoyote kwetu sisi. Kwa hivyo wacha tuangalie hali halisi ya kiroho ya ile laana ya Hamu.

Biblia yanakili, Nuhu alikunywa divai, na katika hali yake ya ulevi, uchi wake ukafunuliwa. Alipokuwa akigaagaa mbele na nyuma, uchi wa ulevi wa divai, mmoja wa wana wake Hamu kwa jina, alimkosea heshima babye na kumdhihaki yeye kwa kwenda kwa nduguze wawili. Wale ndugu zake Hamu walitenda ya hekima na wakatukuza tena baba yao kwa kukosa kuuangalia uchi wake, ila, waliufunika ule uchi. Wakati baba yao ulirudia fahamu zake toka ulevini alimokuwa na kujua yaliyotendeka, alighadhabika na tendo lake Hamu na kumwekelea laana kwa kusema kuwa mwanawe atakuwa mtumwa wa nduguze. Aliwabariki wale wana wengine Shemu na Yafethi na baraka za upanuzi.

Haya yote tuliyoyasoma katika hii laana ya Hamu ni mfano wa kiroho, ambao waweza tu eleweka na wale walio na macho ya kuona na masikio ya kusikia. Huu mfano wafunua siri Yake Mungu wa Kweli na Aishie, Yeye Aliye Hai Pekee, na Ambaye kandoye hamna mwingine. Kulielewa hili fumbo kwafungua macho yetu kuona ile Siri Yake Kristo, Ambaye Ndiye Mfano wa Mungu Asiyeonekana; na huu ndio ufunguo unaotuwezesha kuuvumbua tena na kuuingia Ufalme Wake Mungu mahali ambamo laana ya sheria huisha.

Nuhu katika ulevi na uchi wake aashiria hali ambayo mwanadamu ameanguka kwayo kutoka katika utukufu wa Mungu Baba yake, na kuingilia hali ya muda tu ya utukufu hafifu wa mwanadamu wa kijinsia. Kama unayo macho ya kuona mambo haya ya kiroho utafahamu kuwa  Aliye na Uwepo ni Mungu Baba pekee, na pale mwanzo, kama inawezatafsiriwa vyema, tulikuwa Mmoja Naye. ‘Pale Mwanzo...’ ni mstari unao maana sawa Chanzo cha jambo, kumaanisha kuwa, ule uongo unakuja baadaye kupindua kilichokuwa kweli. Ile hali ya uongo ni ile tutoayo vyanzo vyetu vilivyo ongo visemavyo kuwa sisi tu huru tokana Naye Mungu; ama, kuwa sisi tuna uhai wetu ila Yeye. Yule Trevor, ama Susana, ama Mathayo, ama Mwarabu, Mwamerikani, Mwafrika, Mweupe au Mweusi, ambaye kuamini nilifanywa kuwa, kuanzia siku ile ya uzao wangu ni mvuke tu...kinyago tu...sanamu! Lile umbo nilifanywa kuamini kuwa ndilo nililo, ni mazao ya uongo, na uongo huu umenihuni mie Uzima na Utukufu wa Babangu Mungu.

Kwa kweli, Mungu Ndiye Uzima Wetu...Mawazo Yake ndiyo yangu...Yeye Ndiye sisi...nasi ndio Yeye, na kando Yake hamna mwingine. Mtu atasema, “lakini maneno kama yale ni ya kujikweza tu na ya kiburi pekee!” Wacha niseme kuwa umekosa kupindukia. Kwa kuwa kiburi cha kweli na kujikweza kwenyewe ni kule kuamini kuwa wewe una Uzima wake wewe mwenyewe, ama kuwa kuna uhai mwingine ila Mungu pekee. Kama una hali kama ile ya ya imani, wewe ni mungu kwako wewe mwenyewe, ama kwa njia nyingine pevu zaidi, umejiundia kinyago na sanamu yenye umbo na mfano wako mwenyewe.

Wacha hili likawezekolea ndani, Uzima Wake Mungu, Ambao ndio Uzima pekee, Ndio Uzima pekee ambao Injili ya Kristo imeja kuturejesha Kwake ili tusiishi tena kama wanadamu walioharibiwa kwa kuondolewa kutoka kwenye Uzima wake Mungu, ila tuwe watu waliodhihirika kuwa tu Mmoja Naye. Kila kitu, kiwe cha hali ya kilimwengu, kiungu, kisichoonekana, vyote vyanena kuhusu Umoja wetu Naye Mungu Baba. Mfano mzuri wa Umoja huu wa kiungu waonekana katika matawi na mti yanapokulia; Baba Mungu Ndiye Mti. Nasi ndio Matawi ya Ule Mti. Tawi ni Moja na Mti; Nalo ni uendelezo wa Ule Mti, Ambalo ni dhihirisho la kweli la Hali iliyo ndani Ya Ule Mti, dhihirisho ambalo huonekana kupitia Majani na Matunda ya Lile Tawi. Bila Ule Mti kuwa, Matawi hayaweziota matunda na kuleta mazao; ila hunyauka na kuanguka. Chanzo na Uhai wa Tawi ni Ule Mti, na Tawi haliwezifanya lolote pasipokuwa Mti. Vile vile, katika ile hali, Mti, bila Matawi ambayo huonyesha Hali ya Ule Mti kupitia majani na matunda halina umbo wala maana halisi. Mungu ndiye Mti, ilhali Matawi yaashiria Kristo, Mfano na Umbo Dhahiri Lake Mungu. Kristo Ni MUNGU KATIKA MWANADAMU, ama MUNGU AMEDHIHIRIKA KAMA MWANADAMU. Mungu Asiyeonekana atawezajeonekana na kuwashangaza wana wa Adamu kwa Urembo Wake, na Ukamilifu Wake? Hili lawezekana tu kama atajidhihirisha kupitia Tawi (Kristo) kwa ulimwengu huu. Hii ndio Siri Ya Uungu inayofunuliwa machoni petu siku ya leo: Mungu amedhihirishwa katika Mwili (Kristo/mwanadamu) na kutizamwa kwa mshango na wengi.

Shida ni kuwa yeye mwanadamu ameishi katika upumbavu wa kutojua kweli hii ya kiungu ya kuwa sisi ni Mmoja na Mungu Baba, na upumbavu huu ulio moyoni mwake umemfanya yeye kuishi kama tawi lililotenganishwa na Mti, ambalo hatima yalo ni kifo na kunyauka. Mwanadamu akiishi katika upumbavu huu wa kutoelewa dhamani yake kama Kristo Mwana wa Mungu Ambaye Ni Mmoja na Baba Mungu, yeye ni mfu. Nalo zao ama tunda la kifo na matatizo yaonekanayo katika mwanadamu ni dhihirisho la upumbavu wake kuhusu ile Mbegu ya Mungu Iliyo ndani mwake. Yeye kwa ule upumbavu amevikwa kitani cha uongo na giza la kizazi hiki ili kuwa anapoteza Uzima na Utukufu wa Mungu. Unapowatazama watu wakiishi katika upumbavu ulioko katika kizazi hiki (kutomjua Kristo Aliye ndani mwao) kufuatia miigo waliyoipata kutokana na mawazo ya kimwili yanayofikiriwa na wanadamu walio katika fikra za dhambi na unyonge. Unapowaona wao katika ile hali, unawatazama wana wa Mungu wakiwa katika ulevi wao. Kama divai inavyotia wingu katika ufahamu, kuwa wanadamu wanakosa kutambua nguvu walizo nazo na kuwafanya wapumbavu, vivyo hivyo ndivyo uongo ulioko katika kizazi hiki kilichoko gizani kimeleweshwa kinaposhushika kutoka kwenye Utukufu wa Baba yao kuingilia hali yao ya kijinsia. Tamaa ya macho, tama ya mwili, na kiburi cha maisha kinachotawala ulimwengu huu tulio ni mavuno ya uongo huu ambao wanadamu wameleweshwa kwao. Unaposoma Mithali 23:29-35, utapewa picha ya huyu mwanadamu katika ujuha wake anapoendeshwa toka huku hadi kule katika mawazo yake ya kinyama, tamaa na kutonidhamika kwake kuletako huzuni na uharibifu.

Mithali 23:29-35.
29Ni nani apigaye yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye nguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
30Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; litiapo birauli rangi yake, ishukapo taratibu;
32Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.
33Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.

Wakati mtu amelewa kupindukia, yeye hupoteza fuahamu zake na nidhamu pia. Macho yake huona vinyago na sanamu (mambo ambayo sio Mungu) nay eye huishi katika aibu na kutoheshimika. Huyo sasa ndiye Adamu, anyway uongo wake Shetani. Ulimwengu wote sasa, nikinena kiroho, ni wa giza, na uko chini ya mwongozo wa ile divai na ndio maana wanadamu wagaagaa huku na kule katika aibu na masononeko (1 Wathesalonike 5:4-7). Udhihirisho wa hali zote za chuki na kukosa haki nadhahiri kuwa kuna ulevi wa wale wanaoishi ulimwengu tulio, ambao kwa jina linguine wajulikana kama nje kwenye giza, au jehanamu (Luka 12:45-46).

Kushuka kwake mwanadamu kutoka kwenye Utukufu kwalingana na kuwa na Ile Mbegu yake Mungu ikiwa imetiwa kitani katika giza la ulimwengu huu, ili, kama una upambanuzi moyoni, utamwona Mungu ndani ya kila mwanadamu, bila kujalisha wanavyofanana nje. Mtume Paulo aliipata kweli hii na ndio maana yuasema kuwa, “Simtambui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili..”, ila kwa roho.Kusema kwamba, alikuwa anamwona Kristo ndani ya kila mwanadamu, , sio tu kwa wale waliomkiri kwa kuwa wamezaliwa tena. Alimwona ndani ya KILA MWANADAMU...narudia – KILA MWANADAMU. Wengine yawezekana wesiamke toka usingizini wao katika siku za mwili wao. Lakini hilo halibadilishi ukweli.

2 Wakorintho 5:16Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tulimtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.

Hiyo Mbegu ya Mungu, kama vile tumedhibitisha ni Kristo, Ambaye ni Tawi la Mungu ama Mfano wa Mungu Asiyeonekana, ama bora zaidi, Mungu katika mwanadamu, akijidhihirisha kama mwanadamu. Mwanadamu awaye yote asipotambua hii siri, macho yake ya ufahamu yametiwa upofu kupitia uongo wa kizazi hiki na kwa hivyo chaadhirika kupitia ile laana ya kutengeka kutoka Uzima wake Mungu. Waishio chini ya laana wafanya vile kwa sababu hawautambui Mwili wake Bwana uliohifadhika kama kiotani ndani mwake mwanadamu, ila wanatizama hali ya nje wakitaraji kumwona katika mazingira waliomo. Hii ni hali potovu, na yafanana na kutazama uchi wake Bwana na ni kama kutomheshimu Bwana. Kama utawaona wanadamu kwa jinsi ya mwili wao, na uishi kulingana na hali ya kuona katika mwili, wewe wauona uchi wa Baba na wakosa kumheshimu. Hii yamaanisha kuwa ni lazima tuwe makini zaidi na kuweza pambanua katika roho. Ile kanuni inayonakili, “Mheshimu baba na mama...”, inatimilika tu ndani ya wale ambao wameamka kutoka ulevi wa wanadamu na kuanza kutenda kama Kristo, kwa sababu katika ile hali, utaweza kumtambua Baba ndani mwako na ndani ya ndugu wengine. Katika ufahamu huu, hakuna hatua yoyote inayokwaza kwa sababu katika kweli kuna Mmoja tu ambaye ni Baba ndani ya wote katika yote.

Waefeso 4:6Mungu Mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

 Wakati Yesu alijitwika kitambaa ili kuwaosha wanafunzi wake, Petero alijaribu kukataa, akishindwa ni kwa nini Bwana wake anajishusha chini vile hata kuwaosha miguu yao wanafunzi. Yesu alimjibu kuwa hakungekuwa njia yoyote yeye Petero angeelewa yale aliyoyafanya wakati ule, kwa sababu alikuwa ametiwa kitani cha uongo wa kizazi hichi alichokuwemo. Siri ilikuwa kuwa, kama Yesu alivyojishusha na kuwaosha wanafunzi miguu yao, Alimwona Baba ndani yao, na kazi Yake ilikuwa ni kuwatumikia wao na kuwafanya wao kuamka tena na kurejea katika Utukufu wa Babab yao Mahali ambapo walishuka toka.

Yohana 13:3-7.
3Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, nay a kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
4aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
5Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile litambaa alichofunga.
6Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye...

Yesu zaidi akasema, “Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda”. (Yohana 13:17).

Aliye mkuu kwenu ni Yule awatumikiaye wenzake, sio kama wa mataifa ama waliotiwa kitani, ambao katika upumbavu wao, wajaribu kuwa bwana wa wengine. Ila, mtu akianza kujishusha na kuwa mtumwa, yeye atajipata kuwa bwana na kichwa, na sote twajua Kichwa ni nani – Baba Mungu. Anapojibadili na kumtukuza Baba, atatambua kuwa yeye yu kileleni za Sayuni akitawala na kumiliki kama Babaye.

Kumbukumbu La Torati 28:13Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;

Inamaanisha kuwa ni lazima tubadilike na kufanyika watumwa wa kila mwanadamu, sio kufanyika kama miungu dhidi ya wengine. Kumbuka kuwa, Utukufu tunaoutafuta ni Ule wake Baba, sio wa mwanadamu, tunapotembea katika ufunuo wa Kweli, Anatutukuza sisi na Hali Yake Yeye Mwenyewe, Ambayo nu Ukweli na Dhihirisho la Hali iliyoko pekee. Tofauti kati ya Yesu na mwanadamu wa kawaida ni kuwa, Yesu alitambua kuwa Yeye Alikuwa Mmoja na Mungu Baba kama tunavyotambua wakati huu. Ila, pamoja na ufunuo huu tunaopata, inatubidi kujinyenyekeza na kumtumikia Baba unapomtazama katika wanadamu wote ulimwenguni. Tusipofanya hili, hatutakuwa tumepata ufunuo wa Siri ya Mbegu (Kristo) Yake Baba katika kila mwanadamu.

Wafilipi 2:5-9.
5Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7bali alijifanya juwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa na mfano wa wanadamu;
8tena, alipoonekana an umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
Lolote ndogo utakalowatendea wadogo hawa, utalifanya Kwangu (Baba)...Nilikuwa mwenye njaa ukanipa cha kula...nilikuwa uchi, ukanivisha...nilikuwa korokoroni na ukanitembelea; ingia katika Utukufu na Pumziko katika Mkono wa Kuume wa Baba enyi kondoo wake Bwana (uzao wa Shemu na Yafethi).

Kwa Mkono wa pili wa wana mbuzi (uzao wake Hamu) wanaridhi jehanamu na mauti kama inavyodhihirika kupitia Mkono wa kushoto wake Baba kwa sababu walishindwa kuupambanua Mwili wake Bwana na kuuheshimu.

Mathayo 23:31-34. 31Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaikawatakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
34Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, ufalme mliotengewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

Wanaoonekana kamili na wenye haki ni wale wanaotambua na kuheshimu Milki ya Baba ndani mwao (Kristo) na ndani ya wanadamu wote wapatanao nao, kwa kumkubalisha Yeye kudhihirika toka ndani mwao. Twafanya hili kwa kukataa yale machukizo ya kila aina ya kimwili na uongo wa ulimwengu huu tulio, na kujifuatisha na namna ya Kristo Ambaye Ni Baba (Mungu) ndani mwetu. Hii ndio kweli na uhalali wa Injili: kuwa twapoteza maan yetu katika ulimwengu huu wa mafumbo na mifano na twaungamanika tena na kuwa Mmoja na Baba, kwa kukubalisha Mbegu Yake Kristo (mtu wa kiroho) kukua na kuongezeka ndani mwetu.

Hatima ya mwanadamu  kutembea katika mwili na kutoweza kwake kutambua utukufu wa Umilele na Mungu aliye ndani mwake Asiyeonekana ni kuwa, yeye atakuwa mtumwa wa uharibifu. Usipojijenga katika kuiona na kuitambua Kweli (Kristo ndani mwako) na kujiambatanisha Nayo, wewe utaiona na kutambua kilicho ongo kama Kweli (mwili) na kukitumikia. Kwa maneno mengine, laana yake Hamu ni ishara kwa wanadamu wanaotembea kimwili kwa kufuatia kinachojulikana kijinsia na hatimaje wanashindwa kutambua na kukisadiki kilicho Kweli pekee na Mungu Asiyeonekana Aliye ndani mwao na ndani ya kila mwanadamu. Chini ya laana, mwanadamu hufanyika mtumwa wa kila hali iliyo dhaifu na hafifu ambazo ziliumbwa kumtumikia yeye pale mwanzo.

Unapowaona wanadamu wamefungwa na tama na mavuno ya hali yao ya kimwili, hii ni kwa sababu wamekataa kuhifadhi Yule Mungu wa Kweli Asiyeonekana na wa Uzima wa Milele Aliye ndani mwao, ila wakachagua kutumikia kilichoumbwa, mwili badala ya Muumba (Kristo Aliye ndani). – Warumi 1:20-31. Kifo na uasi vinavyomiliki ulimwenguni, ni matunda tu ya kutotambua Milki yake Mungu ndani ya mwanadamu. Tukiamka kutoka kwenye ulevi ulioko katika kizazi hiki, na kujivika utimamu kupitia Roho wa Kweli, tutatambua kuwa sisi kwa Kweli ni Mwili Mmoja; Mwili wake Kristo Ambao ndio Mwili wake Mungu na Uzima wa Milele (1 Yohana 5:20).

Waefeso 5:18Tena msilewe kwa mvinyo (uongo wa kizazi hiki), ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho (Kweli);

Hatua zake mwanadamu kujaribu kuleta upendo uponyao na amani kupitia kupitia shirika zilizoundwa, tamaduni na shirika za kidini haziwezi kuleta ule upendo upitao maarifa yote. Kile kiletacho Ushirika wa Kweli, Upendo na hatimaye uponyaji wa kila mwanadamu ni uamsho kwa kweli kuwa kuwa Uzima uliopo pekee, ni Uzima wa Mungu Baba. Usipoona utukufu wake Baba ndani ya kila mmoja na kupitia kila mmoja, unao mtizamo uliokataliwa wa Mungu; likiashiria kuwa unauona uchi wake Baba ambao ni laana hata kupitia Torati yake Musa.

Kumbukumbu La Torati 5:16Waheshimu  baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

Mambo Ya Walawi 18:7-8.
7Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue utupu wake.
8Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.
Kama Yesu alivyosema na mtume Paulo akaafikisha, Torati yakamilishwa na neno moja, UPENDO.

Luka 10:27
27Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. (Pia Wagalatia 5:14).

Hili hutimizwa tu ndani mwao pekee wale tu wanaokwea katika utambuzi wao katika na kama Kristo kwa kumtambua Baba ndani ya kila mwanadamu kama Uzima pekee uliopo. Mungu ni Mmoja na Mwili wake ni Mmoja. Wakati divai itakapoisha nguvu zake machoni mwao, watatambua kuwa wako ndani Yake na Yeye Yu ndani mwao. Mtu atasemaje anampenda na kumheshimu Mungu Asiyeonekana wakati hawezi kumpenda na kujiheshimu yeye mwenyewe na nduguye, ambaye katika kweli ni Mungu Anayedhihirika na kutokeza katika umbo la mwanadamu kupitia yeye?

1 Yohana 4:20-21.
20Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
21Na amri hii tumepewa nay eye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.

Wawezaje mbariki Mungu Asiyeonekana na wakati ule ule umlaani mwanadamu ambaye ni mfano wake Mungu? Inatulazimu kuyaosha macho yetu kutokana na wingu la divai kuukuu ya ulimwengu huu iliyotulewesha, ili tukawezemwona Baba aliye ndani ya kila mwanadamu. Mkamilifu ni mtu wa aina gani? Ni Yule awezayeiona Mbegu yake Mungu ndani ya mwanadamu na kuitukuza; Atahifadhi usafi wake na wala hataonja mauti.

Yakobo 3:8-9.
8Bali ulimi hakuna awezaye kuufunga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9Kwa huo twanhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

Wakati Shemu na Yafethi walimtukuza na kumheshimu baba yao kwa kumficha uchi wake, inaashiria utambuzi, kutukuza na upendo. Ni kutembea katika uhusiano na Kweli, kwa kutambua Mungu wa Kweli Asiyeonekana Ambaye ndiye pekee Aliye; Yeye ndiye Aliye ndani mwetu na ndani ya kila mwanadamu. Twapaswa kuwa na jitihada na maakini tunapokutana na wanadamu. Ni kama kukutana kwa kiungu kunakoonekana katika biblia nzima. Mojawapo wa huku kukutana kwa kiungu ni kule Ibrahimu alikopatana naye Bwana kule mialoni ya Mamre; alipoinua macho yake na kuwaona watu watatu waliosimama mbele zake, kwa njia ya kufunguliwa macho na kuona na kupata kutokana na kule kukutana.

Mwanzo 18:1-5.
1Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa amejeti mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
2Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlango pa hema, akainama mpaka chini,
3akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasamimi mtumwa wako.
4Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.
5Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.

Wale watu watatu walitokea katika Jina la Bwana, na sisi twajua kuwa Kristo hufunuliwa katika Jina la Bwana (Ndiye mbarikiwa ajaye kwa Jina la Bwana).Wakati wowote Mungu anapofunuliwa kama mwanadamu, twamtambua kama Kristo, ama Mwana wa Mungu. Sasa twajua kwa nini Yesu asema, kwamba Ibrahimu aliona siku Yake na akaikumbatia kwa furaha na shukrani (Yohana 8:56). Furaha na shukrani ya Ibrahimu kwake Bwana ilionyeshwa kwa kuinama kwake mpaka chini (kuabudu na kusadiki) na kuwatumikia kwa nguvu zake zote na kumtukuza Bwana. Hizi kazi zake Ibrahimu ambazo zilielekea kuzaliwa kwake Isaka, ambaye ni ishara ya Ahadi. Kile tu Ibrahimu alifanya ni kuyainua macho yake na kutambua Uwepo wa Mungu Baba ndani ya hawa watu na hatimaye akapokea Ahadi ya ile Mbegu.

Mbegu ile niishara ya dhihirisho la Kristo, Mfano wake Mungu ndani mwetu, Yeye Ambaye Amebarikiwa na Baraka zake Mungu bila kiwango kutoka vilele vya Milima ya Sayuni.Baraka zake Mungu ni vyote Alivyo navyo na Alivyo.

Tukirejelea Baraka yao Shemu na Yafethi, twaona kuwa yafuata mfano ule ule wa kumtukuza na kumheshimu Baba Aliye ndani mwetu (Kristo ndani mwetu). Tukiutambua Uzima wake Baba ndani mwetu na ndani ya kila mwanadamu na tujishushe na kumkweza Yeye, hatutaona kifo kwa sababu Yeye atukweza pia kupitia Yeye aliye ndani mwetu. Hili  kama Kristo, tutawezaungama kuwa kama umeniona mimi, umemwona Baba, na twajua kuwa katika Baba kuna Uzima wa Milele na hakuna laana yoyote ile.

Yohana 14:8-9.
8Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
9Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wasemaje, Utuonyeshe Baba?

Mwanadamu akiendelea katika hali hii potovu ya kutojijua, akaweze kutambua Utukufu wake Mungu (Vazi Lake Baba), yeye ataupoteza Uzima wake Mungu, na kuridhi ile laana; hili ndilo fumbo lake Hamu. Hebu tafakari maneno haya:

Mwanzo 15:1
1...Mimi (Baba) ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
Yohana 12:26.
26Mtu akinitumikia, na anifuate; name nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Yohana 17:5.
5Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja name, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuweko.

Kufufuliwa ama kupaa ni kukwezwa kule kulikobarikiwa kutoka hali yetu ya kifo na jehanamu tunayojiambatanisha nayo, kurudi kwa utukufu wake Baba, mahali ambapo uoga, hofu, hali ya kukosa na kuachwa vyatokomea. Katika utukufu wake Baba, kifo hakimo tena kwa sababu, ndani Yake Baba hamna kifo, ila furaha, faraja, kicheko ambacho chafanyika chetu milele yote.

Isaya 51:11.
11Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.

Wale watakaoingia malango ya Yerusalemu Mpya ambayo kwa jina linguine yajulikana kama Ufalme wa Mungu, ambayo ni hali ya utambuzi tunayoipata ndani mwetu, mahali ambamo hamna giza wala laana, wafanya vile kwa kuuangalia Uso wake Baba kwa imani na kumtumikia Yeye. Hawa hawawezirudi tena wala kurejea tena katika hali duni na dhaifu ya wanadamu, na wanaungamanika na Utukufu wake Mungu, kama inavyoonekana kupitia Majina ya Baba kwenye vipaji vyao.

Ufunuo wa Yohana 22:3-5.
3Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;
4nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.
5Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.

Vilevile, wale waeneao kupitia uongo wa kiwanadamu kwa kukataa kutambua Baba na kumtukuza Yeye, watabaki nje ya malango ya ule mji wa kibingu wa nuru.

Ufunuo wa Yohana 22:15.
15Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauwaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Hii ndio hali ya mataifa ya ulimwengu huu leo; wale ambao nia zao zimetiwa giza kwa ule ubatili wa kizazi hiki na kwa hiyo hawawezitambua hii siri ya Utukufu wake Baba (Kristo) aliyefichika ndani ya mwanadamu.

Muda na wakati tuliomo (wakati huu unaoendelea), Mungu anatuma roho wa Eliya ili kuleta kutubu na kurejea kutoka njia zetu tulizo, ambazo hazimtukuzi Baba. Roho wa Eliya aleta urejesho wa njia yake Bwana ndani mwetu jinsi ilivyokuwa pale mwanzo.Kama tunavyosoma katika maandiko, Mithali 30:17...Kunguru wa bondeni...ambayo ni ishara ya sauti ya Yule aliaye nyikani (Eliya) yalia leo ili kung’oa jicho ovu lake mwanadamulinalomfanya yeye kudhihaki na kuto,heshimu Baba na Mama (Kristo na Kanisa).

Mithali 30:17.
17Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila.
Hawa ndio mashahidi wa Kweli wa Mungu wanaofunua Ukweli, ili moyo wa Baba ukawarejelee wana na wana kwake Baba.

Malaki 4:5-6.
5angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.
6Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.

Hii ni kuhusu kuwarejesha wote kuwa Mmoja katika Baba, vile tulivyo toka mwanzo. Watu wote (matawi), lazima yaunganishwe tena katika ule Mti ndio tena wakawezejitwaalia tena kutoka Uzima wa ule Mti (Mungu Baba) na wakawezetoa mazao kufuatia kule kungamanika. Hili litagharimu kauli na mkazo kwao watakatifu wanaoupokea huu ufunuo wake Baba kati ya maumbile yake. Inamaanisha kujiona maisha yetu katika ulimwengu huu kama kitu dhaifu na kinyonge, ili kuuacha ule uhai wa kilimwengu na kupokea Utukufu wake Baba.

Baraka Kwenu.
Trevor Eghagha

trevor@sunrayministry.org

www.sunrayministry.org